MWANAUME USIOE MKE KWA AJILI YA WATU WENGINE, kutana na mwl Edward
SOMO : MWANAUME USIOE MKE KWA AJILI YA WATU WENGINE
MWL: EDWARD KISUSU
Shalom shalom acha leo ni wakumbushe wanaume wote ambao wameoa ama hawajaoa na wale wanaohitaji kuoa *USIOE MKE KWA AJILI YA WATU WENGINE*
kuna baadhi ya wanaume wanaoa mke kwa ajili ya watu wengne 
*Zifuatazo ni dalili na mambo ya mwanaume aliyeoa mke au anayetaka kuoa kwa sababu ya watu wengne*
*Dalili 1. HUCHAGUA SANA SURA,SHEPU NA RANGI*
hii ni dalili namba 1 ambayo imechukua nafas kubwa kwa mwanaume anayeoa kwa ajili ya wengne hutafuta mwanamke mzuri mwenye shepu nzuri na rangi angavu ili kila anapopita watu wamsifie waseme kweli jamaa ameoa mwanamke Mzuri sana dah 
*Dalili 2.HUPENDA SIFA SANA*
mwanaume aliyeoa mke kwa ajili ya watu hupenda sifa sana hata akikaa mahali yeye huwa kazi yake ni kuponda wake za wanaume wenzake kuwa walikosea kuoa wameoa wanawake wabaya hata huogopa kutembea nao mitahani na mambo mengi humsifia mke wake ambaye mtaa mzima hutangaza ni mzuri
*Dalili 3. KABLA YA NDOA HUWA NA MAJIGAMBO SANA*
hapa ndio utagundua huyu mtu anaoa kwa ajili ya watu ataanza kumpost mitandao yote na kuhoji kama ni mzuri ama la kila anayekutana nae iwe sokon njian atauliza mchumba wangu umemuona?? Mzuri au mbaya nipe maksi ebu 
*Dalili 4. HUTAFUTA USHAUR SANA*
mwanaume mwenye silika na hulka za kuoa kwa ajili ya watu Hutapatapa sana kutafuta ushaur kwa watu weng na kikubwa huoji je mwanamke huyu ni mzuri?? Vip shepu yake nipe maksi basi ngap unampa figure yake vipi Elimu yake unaionaje??
*Dalili 5. KUCHUMBIA NA KUACHA*
kwa leo tutamalizia na sababu hii kubwa kuliko zote sasa imekuwa kero wanaume siku za leo wanachumbia na kuacha sababu kubwa ni *NI KUOA KWA AJILI YA WENGNE* kwenye dalili hii wanaume weng huchumbia ila huanza kuskiliza maneno ya watu mara ooh miguu kama miwa sura kama anazma mshumaa hana hadhi ya kuwa na ww hapo mwanaume anayeoa kwa ajili ya wengne hujikuta ANACHUMBIA KILA SIKU NA KUACHA KILA SIKU 
*MADHARA YA KUOA KWA AJILI YA WATU WENGNE*
*1. KUOA MTU ASIYE SAHIHI*
ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni kwa ajili ya watu unajikuta unaoa mwanamke asiye makusudi ya Mungu ndoa yako inakuwa kama kaburi nje imepambwa vyema na mashada na tiles inapendeza kumbe ndani mifupa mikavu iliyooza
*2. KUWA MTUMWA*
wanaume wa namna hii hukutana na utumwa mzito ndani ya ndoa zao kwa maana alilazimisha maji kupanda mlima kwa maneno ya watu ukachagua mwanamke mzur asiye na adabu anayejiona kupita malaika wa mbinguni
*3. NDOA KUVUNJIKA*
kwa mabango na vijembe vya ndani ya ndoa hufanya ndoa nying za wanaume wapenda sifa kuisha kabisa na kuvunjika kwa kuoa mtu asiye wako
*4. UGOMVI WA FAMILIA*
hapa ndio utaona madhara makubwa kwa kujikuta unagombana na familia yako yote kwa kuoa mwanamke asiye na maadili na kusababisha ugombane na familia yako kwa gubu lake kwa ndugu jamaa na marafiki 
*5. KUTOFAUTIANA NA JAMII*
kwa maneno na hali ya hewa kachafuka watu weng hujikuta hata jamii inawachukia na kukosa sapot kwa jamaa na jamii kwa ujumla
*HITIMISHO:* Sio kwamba kuoa mwanamke mzuri na shep nzur na rangi ni dhambi la hasha si dhambi wala si makosa ila muhimu kujua unaoa ili iweje je huyo mwanamke mzuri anaishi na nani na watu ama na ww muoaji je Tabia zake zinasemekanaje na jamii je ni Mpango wa Mungu mimi kumuoa huyu dada?? Hayo ndio maswali ya kujiuliza usioe kwa sababu watu waone na wewe umeoa mwanamke mzuri noooo huo ni upuuuzi oa mwanamke atakayekufaa kwenye maisha yako acha kufuata mkumbo Fulan kaoa mwanamke mzuri shepu nzur na ww unaiga acha mashindano ndoa sio mashindano ya magar nani ana gari zur kuliko mwenzake *TAFAKARI MWANAUME CHUKUA HATUA*
*MWL.EDWARD KISUSU*
WHATSAPP 0764899489
INSTA *@edwardkisusu*
 
Sana
ReplyDelete