Kutana na mr Deo Simulizi ya SHIDA ZA MATAJIRI

SHIDA ZA MATAJIRI (the Rich's broblems)  -01
Deo Massawe,+255769297430.

Ikiwa ni siku ya thelathini na tisa tangu Bahati azaliwe baba yake aliendelea kuumia ndani ya moyo wake kwani aliwaza ni kwa jinsi gani angeweza kumtoa mwanae sadaka,
"mimi  na mke wangu Janeth tumeteseka kwa miaka mitatu tukitafuta mtoto,sasa tumempata na anastahili kutolewa sadaka,nitafanyaje?" alijisemea baba bahati.
Mda ulizidi kusogea hatimae pakapambazuka,mama bahati aliamka na kwa haraka aliingia bafuni,kwani siku hiyo ilikua aende hospital huku nae baba Bahati akihitajika kufanya mauajia ya mtoto huyo ili asalie na utajiri aliokua nao.
                 *****
Kwa upendo Janeth aliokua nao kwa mwanae basi kila alipokua anatoka  chumbani alihakikisha anashusha chandarua.
  Watoto wa jirani mara  nyingi waliwahi nyumbani kwa Brayson ambae ndio baba wa Bahati, walicheza michezo mbali mbali ndani ya nyumba ya baba Bahati,siku hiyo walikua wakicheza mchezo wakujificha,yaani mmoja anajificha kisha kutafutwa.
                 *****
"Mungu nisaidie kwa kosa hili kwani naenda kuua kiumbe asiye na hatia" Brayson alijisemea huku akipiga hatua  kuelekea chumba alicholazwa mwanae alifanya kwa haraka ili mkewe aliyekua bafuni akitoka akute kila kitu kimekamilika. Alianua chandarua kwa haraka akamtoa Bahati akambusu kisha kuelekea naye chumba kilichokua na Jokofu ( freezer) kubwa la  kugandisha barafu.
"nitamuweka humu afe  taratibu" alisema Brayson huku akifungua mlango wa  jokofu hilo uliokua  wa kuinua.
                ******
Ndani ya chumba alichokua Brayson akitekeleza mauaji ya mtoto wake Bahati kulikua na mtoto mmoja aliyejificha nyuma ya mlango kwa ajili ya michezo yao waliyokua wakifanya lakini baba Bahati hakujua kama chumbani hapo pangeweza kua na mtu.
"acha baba ataganda kama ice cream" ni sauti iliyopenya masikioni mwa Brayson alivyomtumbukiza mtoto ndani ya jokofu,Brayson aligeuka nyuma na kuona sura ya mtoto wa jirani na kwa haraka alisitisha kitendo hicho na kuingia haraka chumbani kwake na kutoa bastola kisha kumuua yule mtoto wa jirani.
Aneth aliyekua bafuni alitoka haraka bila hata kujifunga kanga kwani mlio wa bunduki ulidhihirisha hatari nyumbani hapo.
"jamani mwananguuuuu" Janeth alipiga kelele huku akitaja jina la mwanae......

Ili kupata mwendelezo wa hadithi hii unatakiwa kugharamia shilingi mia tatu, kisha utatumiwa moja Kwa moja katika inbox yako ya WhatsApp, e-mail, messenger, au Twitter. Nitumie  namba yako inbox ili uweze kuipata yote. Ni hadithi nzuri yenye kusikitisha na kufundisha sana.

Comments

Amani Fredy

SUA: SIFA ZA KUJIUNGA NA CHUO KWA KILA KOZI 2017/2018

RATIBA YA TIGO FIESTA 2017 NA LIST YA WASANII WATAKAOKUWEPO (TUMEKUSOMA)